Quran in Swahili Al-Fîl 105 – AL – FIILKWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?2. Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?3. Na akawapelekea ndege makundikwamakundi, 4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,5. Akawafanyakamamajani yaliyo liwa!