93 – WADH-DHUH’AA
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Naapakwamchana!
- 2. Nakwausiku unapo tanda!
- 3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
- 4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
- 5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
- 6. Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
- 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa?
- 8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
- 9. Basi yatima usimwonee!
- 10. Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
- 11. Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.