Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Al-ʽAdiyât

100 – AL – A’ADIYAAT

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

 1. 1. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
 2. 2. Na wakitoa motokwakupiga kwato zao chini, 
 3. 3. Wakishambulia wakati wa asubuhi,
 4. 4. Huku wakitimua vumbi,
 5. 5. Na wakijitoma kati ya kundi,
 6. 6. Hakika mwanaadamunimtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! 
 7. 7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shakanishahidi wa hayo! 
 8. 8. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupendamali!
 9. 9. Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
 10. 10. Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
 11. 11. Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwanakhabari zao wote!