Quran in Swahili
Al-ʽAlaq
96 – AL – A’LAQ
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
- 2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
- 3. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
- 4. Ambaye amefundisha kwa kalamu.
- 5. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
- 6. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
- 7. Akijiona katajirika.
- 8. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
- 9. Umemwona yule anaye mkataza
- 10. Mja anapo sali?
- 11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
- 12. Au anaamrisha uchamngu?
- 13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
- 14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
- 15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
- 16. Shungi la uwongo, lenye makosa!
- 17. Basi na awaite wenzake!
- 18. Nasi tutawaita Mazabania!
- 19. Hasha! Usimt’ii! Nawe sujudu na ujongee!