Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Al-Aʽlâ

87 – AL – AA’LAA

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

  1. 1. Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
  2. 2. Aliye umba, na akaweka sawa,
  3. 3. Na ambaye amekadirianaakaongoa, 
  4. 4. Na aliye otesha malisho,
  5. 5. Kisha akayafanya makavu, meusi.
  6. 6. Tutakusomesha wala hutasahau,
  7. 7. Ilaakipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahirina yaliyo fichikana. 
  8. 8. Na tutakusahilishia yawe mepesi.
  9. 9. Basi kumbusha,kamakukumbusha kunafaa. 
  10. 10. Atakumbuka mwenye kuogopa.
  11. 11. Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
  12. 12. Ambaye atauingia Moto mkubwa.
  13. 13. Tena humo hatakufa wala hawi hai.
  14. 14. Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
  15. 15. Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
  16. 16. Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
  17. 17. Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
  18. 18. Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
  19. 19. Vitabu vya Ibrahimu na Musa.