Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Al-Anʽâm

6 – AL – AN-A’AM

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

 1. 1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi,naakafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na Mola wao Mlezi. 
 2. 2. Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha akakuhukumieni ajali,namuda maalumu uko kwake tu. Tena baada ya haya nyinyi mnatia shaka. 
 3. 3. Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbingunina Anajua ya ndani yenu na ya nje yenu. Na anajua mnayo yachuma. 
 4. 4. Na haiwafikii hata ishara moja katika ishara za Mola wao Mleziilawao huwa wenye kuipa nyongo. 
 5. 5. Wameikanusha Haki ilipo wajia.Basi zitawajia khabari zayalewaliyo kuwa wakiyakejeli. 
 6. 6. Jee, hawaoni vizazi vingapi tulivyo viangamiza kablayao? Tuliwaweka katika nchi tusivyo kuwekeni nyinyi; tukawapelekea mvua nyingina tukaifanya mito inapita chini yao. Mwishoe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yaokizazi kingine. 
 7. 7. Na lau tungeli kuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusakwa mikono yao, wangeli sema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uchawi dhaahiri.
 8. 8. Na wao husema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Nakamatungeli teremsha Malaika, basi bila ya shaka ingesha hukumiwa amri, tena hapo wasingeli pewa muhula.
 9. 9. Nakama tungeli mfanya Malaika bila ya shaka tungeli mfanya kamabinaadamu, na tungeli watilia matatizo yale wanayo yatatiza wao. 
 10. 10. Na hakika Mitume walio kabla yako walifanyiwa kejeli, lakini walio wafanyia kejeli wakaja kuzungukwanayale yale waliyo kuwa wao wanayafanyia kejeli. 
 11. 11. Sema: Tembeeni ulimwenguni, kisha mtazame ulikuwaje mwishowawanao kanusha. 
 12. 12. Sema: Ni vya nani viliomo katika mbingunakatika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye amejilazimisha nafsi yake kurehemu. Hakika atakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo kuwa na Walio jikhasiri wenyewe hawaamini. 
 13. 13. Nanivyake vilio tulia usiku na mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. 
 14. 14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingunaardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wakwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa 
 15. 15. Sema: Mimi naogopa adhabu ya Siku kubwa hiyo ikiwa nitamuasi Mola wangu Mlezi.
 16. 16. Siku hiyo yule atakaye epushwa nayo adhabu hiyo atakuwa Mwenyezi Mungu amemrehemu.Na huko ndiko kufuzu kulio wazi.
 17. 17. Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapanawakukuondolea hayo ila Yeye. Na ikiwa akikugusisha kheri, basi Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu. 
 18. 18. Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake,nandiye Mwenye hikima na Mwenye khabari zote. 
 19. 19. Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yanguna Na nimefunuliwa Qur’ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja naMwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha. 
 20. 20. Wale Tulio wapa Kitabu wanayajua hayakamawanavyo wajua watoto wao. Wale walio zikhasiri nafsi zao hawaamini. 
 21. 21. Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu,naakazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi. 
 22. 22. Siku tutapo wakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie walio shirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mlio kuwa mnadai?
 23. 23. Kisha hautakuwa udhuru waoilani kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina. 
 24. 24. Tazama jinsi wanavyo jisemea uwongo wenyewe.Na yamewapotea waliyo kuwa wakiyazua.
 25. 25. Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza;natumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kwakujadiliana nawe, wanasema walio kufuru: Hizi si chochote ila hadithi za watu wa kale. 
 26. 26. Nao huwazuia watu,nawao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu, wala wao hawatambui. 
 27. 27. Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi,natutakuwa miongoni wa Waumini. 
 28. 28.Baliyamewadhihirikia waliyo kuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangeli rudishwa bila ya shaka wange yarejea yale yale waliyo katazwa. Na hakika hao ni  
 29. 29. Na walisema: Hakuna mengineilamaisha yetu haya ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa. 
 30. 30. Na lau ungeli ona watavyo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akawaambia: Je, si kweli haya?Na wao watasema: Kwani? Tunaapakwa Mola Mlezi wetu ni kweli. Yeye atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyo kuwa mnakataa. 
 31. 31. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetukwatuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba. 
 32. 32. Na maisha ya dunia si chochteilani mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini? 
 33. 33. Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha wanayo yasema. Basi hakika wao hawakukanushi wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
 34. 34. Na hakika walikanushwa Mitumewakabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu. Na hapana wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na bila ya shaka zimekujia baadhi ya khabari za Mitume hao. 
 35. 35. Na ikiwani makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwachini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara — Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua. 
 36. 36. Hakika wanao kubaliniwale wanao sikia. Na ama wafu Mwenyezi Mungu atawafufua, na kisha kwake Yeye ndio watarejeshwa. 
 37. 37. Na wamesema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutokakwaMola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu niMuweza wa kuteremsha muujiza. Lakini wengi wao hawajui. 
 38. 38. Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye rukakwambawa zake mbili, ila ni ummakama  Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa. 
 39. 39. Na walio kanusha Ishara zetuniviziwi na mabubu waliomo gizani. Mwenyezi Mungu humwachia kupotea amtakaye, nahumweka katika Njia iliyo nyooka amtakaye. 
 40. 40. Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa – mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyiniwakweli? 
 41. 41. Bali Yeye ndiye mtakaye mwomba, naye atakuondoleeni mnacho mwombea akipenda.Na mtasahau hao mnao wafanya washirika wake.
 42. 42. Nakwa yakini tulipeleka Mitume kwakaumu zilizo kuwa kabla yako, kisha tukazitia katika dhiki na mashaka ili zipate kunyenyekea. 
 43. 43. Kwa nini wasinyenyekee ilipo wafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu,naShet’ani akawapambia waliyo kuwa wakiyafanya. 
 44. 44. Basi walipo sahau walio kumbushwa tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipo furahiayale waliyo pewa tuliwashika kwaghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa. 
 45. 45. Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu – na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola Mleziwaviumbe vyote. 
 46. 46. Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akanyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu,nimungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni hayo tena? Angalia vipi tunavyo zieleza Ishara, kisha wao wanapuuza. 
 47. 47. Sema: Mwaonaje, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungukwaghafla, au kwa dhaahiri, jee wataangamizwa isipo kuwa walio dhulumu? 
 48. 48. Na hatuwatumi Mitumeilahuwa ni wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. 
 49. 49. Na walio kanusha Ishara zetu itawagusa adhabukwawalivyo kuwa wakipotoka. 
 50. 50. Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu.Wala sijui mambo yaliyo fichikana.Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri? 
 51. 51. Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywakwaMola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu.
 52. 52. Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhinajioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu. 
 53. 53. Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu waokwawao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanao shukuru? 
 54. 54. Na wanapo kujia wanao ziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakaye fanya uovu miongoni mwenukwaujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. 
 55. 55. Na ndio hivi tunavyo zieleza Isharailiibainike njia ya wakosefu. 
 56. 56. Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu. Sema:mimisifuati matamanio yenu. Hivyo nitakuwa nimepotea, na sitakuwa miongoni mwa walio ongoka. 
 57. 57. Sema: Mimi nipo kwenye sharia iliyo wazi itokayokwaMola wangu Mlezi, nanyi mnaikanusha. Mimi sinacho hicho mnacho kihimiza. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote. 
 58. 58. Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnacho kihimiza, ingeli kwisha katwa shauri baina yanguna Na Mwenyezi Mungu anawashinda wote kuwajua madhaalimu. 
 59. 59. Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuayeilaYeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na  Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha. 
 60. 60. Naye ndiye anaye kufisheni usiku,naanakijua mlicho fanya mchana. Kisha Yeye hukufufueni humo mchana ili muda ulio wekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu, na tena akwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. 
 61. 61. Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na hukupelekeeni waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.
 62. 62. Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola waowa Hakika, hukumuni yake. Naye ni Mwepesi kuliko wote wanao hisabu. 
 63. 63. Sema: Ni nani anaye kuokoeni katikagizala nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru. 
 64. 64. Sema: Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka hayo, na kutoka kila mashaka,nakisha nyinyi mnamshirikisha! 
 65. 65. Sema: Yeye ndiye Muwezawakukuleteeni adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au kukuleteeni fujo la mfarakano, na kuwaonjesha baadhi yenu jeuri ya wenzao. Tazama vipi tunavyo zieleza Aya ili wapate kufahamu. 
 66. 66. Na watu wako wameikanusha, nayoni Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu. 
 67. 67. Kila khabariinakipindi chake. Nanyi mtakuja jua. 
 68. 68. Na unapo waona wanao ziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. NakamaShet’ani akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu. 
 69. 69. Wala wamchao Mungu hawana jukumu lolote kwao, lakini ni kukumbusha, asaa wapate kujiepusha.
 70. 70. Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao,nauhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo yachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingatoa kila fidia haitokubaliwa. Hao ndio walio angamizwa kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu. 
 71. 71. Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru,naturejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet’ani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi waviumbe vyote, 
 72. 72. Na mshike Sala,namcheni Yeye, na kwake Yeye ndiko mtako kusanywa. 
 73. 73. Naye ndiye aliye ziumba mbingunaardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni  Na ufalme wote ni wake Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye ndiye Mwenye hikima naMwenye khabari. 
 74. 74. Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwanimiungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mmo katika opotofu ulio wazi. 
 75. 75. Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalmewa mbingu naardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini.
 76. 76. Na ulipo muingilia usiku akiona nyota, akasema: HuyuniMola Mlezi wangu. Ilipo tua akasema: Siwapendi wanao tua.
 77. 77. Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema:KamaMola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea. 
 78. 78. Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu.Huyu mkubwa kuliko wote.Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina. 
 79. 79. Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, walamimisi miongoni mwa washirikina. 
 80. 80. Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu,nahali Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi akipenda kitu.Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki? 
 81. 81. Na vipi nivikhofu hivyo mnavyo vishirikisha, hali nyinyi hamkhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungunakitu ambacho hakukiteremshia uthibitisho. Basi kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani,kama nyinyi mnajua? 
 82. 82. Wale ambao wameamini,nahawakuchanganya imani yao na dhulma – hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka. 
 83. 83. Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiananawatu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi. 
 84. 84. Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haqna Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema. 
 85. 85. Na ZakarianaYahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema. 
 86. 86. Na Ismail,na Al Yasaa, naYunus, na Lut’. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu wote. 
 87. 87. Na kutokananababa zao, na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawateuwa na tukawaongoa kwenye Njia iliyo nyooka. 
 88. 88. Hiyonihidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda. 
 89. 89. Hao ndio tulio wapa Vitabunahukumu na Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa. 
 90. 90. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidayayao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwaila ni mawaidha kwa walimwengu wote. 
 91. 91. Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungukwahaki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlicho kifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu?Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache wacheze katika porojo lao. 
 92. 92. Na hikiniKitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao. 
 93. 93. Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi;nahali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremshakama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake. 
 94. 94. Nanyi mlitujia wapwekekamatulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai. 
 95. 95. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye hai kutoka maiti, nayenimtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa? 
 96. 96. Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na utulivu,najua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi. 
 97. 97. Na Yeye ndiye aliye kuwekeeni nyotailimwongoke kwazo katika kiza cha bara na bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizikwa watu wanao jua. 
 98. 98. Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokanananafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu. 
 99. 99. Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni;nakwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokanana baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake punje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, namakomamanga, yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na  Hakika katika hayo pana Ishara kwa watu wanao amini. 
 100. 100. Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake,nahali Yeye ndiye aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo mbandikiza nayo! 
 101. 101. Yeye ndiye Muumbajiwambingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu. 
 102. 102. Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumbawakila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu. 
 103. 103. Macho hayamfikiliibaliYeye anayafikilia macho. Naye niMjuzi, Mwenye khabari. 
 104. 104. Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutokakwaMola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu. 
 105. 105. Na namna hivyo tunazisarifu Aya,nawao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanao jua. 
 106. 106. Fuata uliyo funuliwa kutokakwaMola wako Mlezi. Hapana mungu ila  Na jitenge na washirikina. 
 107. 107. Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki.Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao.Wala wewe si mlinzi juu yao. 
 108. 108. Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasijenawao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda. 
 109. 109. Na waliapakwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo waviapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara wataiamini. Sema: Ishara ziko kwaMwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa zitapo kuja hawato amini. 
 110. 110. Nasi twazigeuza nyoyo zaonamacho yao. Kama walivyo kuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao  
 111. 111. NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika,na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake.Lakini wengi wao wamo ujingani. 
 112. 112. Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet’aniwa kiwatu, nakijini, wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli penda Mola wako Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na wanayo yazua. 
 113. 113. Nailinyoyo za wasio amini Akhera zielekee hayo, nao wayaridhie na wayachume wanayo yachuma. 
 114. 114. Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwanaMola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanaotia  
 115. 115. Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wakokwakweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. 
 116. 116. Na ukiwat’ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupotezanaNjia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati iladhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu. 
 117. 117. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio potea Njia yake,nandiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio hidika. 
 118. 118. Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake.
 119. 119. Nakwanini msile katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua wanao pindukia mipaka. 
 120. 120. Na acheni dhambi zilizo dhaahirinazilizo fichikana. Hakika wanao chuma dhambi watalipwa kwa waliyo kuwa wakiyachuma. 
 121. 121. Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huoni Na kwa yakini mashet’ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina. 
 122. 122. Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wakenikama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya. 
 123. 123. Kadhaalika katika kila mji tumewajaalia wakubwawawakosefu wao wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipo kuwa nafsi zao, nao hawatambui.
 124. 124. Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfanowawalio pewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya. 
 125. 125. Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chakekwa Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini. 
 126. 126. Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi Iliyo nyooka. Tumezipambanua Ayakwawatu wanao kumbuka. 
 127. 127. Hao watapata nyumba ya salamakwaMola Mlezi wao. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyatenda. 
 128. 128. Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini!Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu.Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na  Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua. 
 129. 129. Ndiokamahivi tunawaelekeza madhaalimu wapendane wao kwa wao kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyachuma. 
 130. 130. Enyi makundi ya majininawatu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri. 
 131. 131. Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa wa kuiangamiza miji kwa dhulma, hali wenyewe wameghafilika.
 132. 132. Na wote wana daraja mbali mbali kutokananayale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda. 
 133. 133. Na Mola wako Mlezi ndiye Mkwasi, Mwenye rehema. Akipenda atakuondoeninaawaweke wengine awapendao badala yenu, kama vile alivyo kutoeni kutokana na uzazi wa watu wengine. 
 134. 134. Bila ya shaka hayo mnayo ahidiwa yatafika tu, wala nyinyi hamtaweza kuyaepuka.
 135. 135. Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo,nahakika mimi nafanya. Mtakuja jua nani atakuwa na makaazi mema mwishoni. Hakika madhaalimu hawatafanikiwa. 
 136. 136. Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimeanawanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu – kwa madai yao – na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Mwenyezi Mungu, na vilivyo kuwa vya Mwenyezi Mungu huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu.  
 137. 137. Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwauwa watoto waoilikuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda wasinge fanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua. 
 138. 138. Nao husema: Wanyama hawanamimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao – kwa madai yao  Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao. Wanamzulia uwongo tu Mwenyezi Mungu. Atawalipa kwa hayo wanayo mzulia. 
 139. 139. Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawanikwa ajili ya wanaume wetu tu, na wameharimishwa kwa wake zetu.Lakini ikiwa nyamafu basi wanashirikiana. Mwenyezi Mungu atawalipa kwa maelezo yao  Hakika Yeye niMwenye hikima, Mwenye kujua. 
 140. 140. Hakika wamekhasirika wale ambao wamewauwa watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua,nawakaharimisha alivyo waruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu. Hakika wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka. 
 141. 141. Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja,na zisio tambaa, na mitende, namimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa  Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo. 
 142. 142. Na katika wanyama amekujaalieni wenye kubeba mizigonakutoa matandiko. Kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shet’ani. Hakika yeyeni adui yenu dhaahiri. 
 143. 143. Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo,nawawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli. 
 144. 144. Na wawili katika ngamia,nawawili katika ng’ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu. 
 145. 145. Sema: Sioni katikayaleniliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi niMwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 
 146. 146. Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng’ombena kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyokwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli. 
 147. 147. Wakikukanusha basi wewe sema: Mola Mlezi wenuniMwenye rehema iliyo enea. Wala haizuiliki adhabu yakekwawatu wakhalifu. 
 148. 148. Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kablayaompaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila  Wala hamsemi ilauwongo tu. 
 149. 149. Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Nakamaangeli penda angeli kuhidini nyote. 
 150. 150. Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera,naambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine. 
 151. 151. Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayonikuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na  Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ilimyatie akilini. 
 152. 152. Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimonamizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ilimpate kukumbuka. 
 153. 153. Nakwahakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu. 
 154. 154. Tena tulimpa Musa Kitabukwakumtimizia (neema) aliye fanya wema, na kuwa ni maelezo ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili wapate kuamini mkutano wao na Mola wao Mlezi. 
 155. 155. Na hichiniKitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mchenimngu, ili mrehemewe. 
 156. 156. Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu;nasisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma. 
 157. 157. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutokakwa Mola wenu Mlezi, nauwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao. 
 158. 158. Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.
 159. 159. Hakika walio igawa Dini yao na wakawa makundi makundi, huna ukhusiano nao wowote. Bila ya shaka shauriyaoiko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawaambia yale waliyo kuwa wakiyatenda. 
 160. 160. Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi.naafanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa. 
 161. 161. Sema: Kwa hakikamimiMola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. 
 162. 162. Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mleziwaviumbe vyote.
 163. 163. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa,namimi ni wa kwanza wa Waislamu.
 164. 164. Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu,nahali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana. 
 165. 165. Naye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa,iliakujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu