Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Al-Fâtihah

1 – AL-FAATIH’A

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

  1. 1. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
  2. 2. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mleziwaviumbe vyote; 
  3. 3. MwingiwaRehema Mwenye Kurehemu; 
  4. 4. Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
  5. 5. Wewe tu tunakuabudu,naWewe tu tunakuomba msaada. 
  6. 6. Tuongoe njia iliyo nyooka,
  7. 7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.