105 – AL – FIIL
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
- 2. Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
- 3. Na akawapelekea ndege makundikwamakundi,
- 4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
- 5. Akawafanyakamamajani yaliyo liwa!