Quran in Swahili
Al-Hâqqah
69 – AL – H’AAQQAH
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Tukio la haki.
- 2. NinihiloTukio la haki?
- 3. Na nini kitakujuulisha ninihiloTukio la haki?
- 4. Thamudi na A’di waliukadhibisha Msiba unao situsha.
- 5. Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
- 6. Na ama A’di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.
- 7. Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepindukakamakwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
- 8. Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?
- 9. Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia.
- 10. Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
- 11. Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina,
- 12.Ilituyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi.
- 13. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,
- 14. Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja,
- 15. Siku hiyo ndio Tukio litatukia.
- 16. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
- 17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.
- 18. Siku hiyo mtahudhurishwa – haitafichika siri yoyote yenu.
- 19. Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
- 20. Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.
- 21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza,
- 22. Katika Bustani ya juu,
- 23. Matunda yake yakaribu.
- 24. Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.
- 25. Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!
- 26. Wala nisingeli jua nini hisabu yangu.
- 27. Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.
- 28.Maliyangu hayakunifaa kitu.
- 29. Madaraka yangu yamenipotea.
- 30. (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!
- 31. Kisha mtupeni Motoni!
- 32. Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!
- 33. Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu,
- 34. Wala hahimizi kulisha masikini.
- 35. Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,
- 36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
- 37. Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
- 38. Basi naapa kwa mnavyo viona,
- 39. Na msivyo viona,
- 40. Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
- 41. Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machachesanamnayo yaamini.
- 42. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
- 43. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 44. Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,
- 45. Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,
- 46. Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
- 47. Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.
- 48. Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.
- 49. Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
- 50. Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
- 51. Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
- 52. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.