104 – AL – HUMAZAH
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Ole wake kila safihi, msengenyaji!
- 2. Aliye kusanyamalina kuyahisabu.
- 3. Anadhani ya kuwamaliyake yatambakisha milele!
- 4. Hasha!Atavurumishwa katika H’ut’ama.
- 5. Na nani atakujuvyaninini H’ut’ama?
- 6. MotowaMwenyezi Mungu ulio washwa.
- 7. Ambao unapanda nyoyoni.
- 8. Hakika huo utafungiwa nao
- 9. Kwenye nguzo zilio nyooshwa.