Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Al-Layl

92 – AL – LAYL

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

 1. 1. Naapakwausiku unapo funika! 
 2. 2. Na mchana unapo dhihiri!
 3. 3. NakwaAliye umba dume na jike! 
 4. 4. Hakika juhudi zenu bila ya shakanimbali mbali. 
 5. 5. Ama mwenye kutoanaakamchamngu, 
 6. 6. Na akaliwafiki lilio jema,
 7. 7. Tutamsahilishia yawe mepesi.
 8. 8. Na ama mwenye kufanya ubakhili,na asiwe nahaja ya wenzake, 
 9. 9. Na akakanusha lilio jema,
 10. 10. Tutamsahilishia yawe mazito!
 11. 11. Namaliyake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? 
 12. 12. Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
 13. 13. Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
 14. 14. Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
 15. 15. Hatauingia ila mwovu kabisa!
 16. 16. Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
 17. 17. Na mchamngu ataepushwa nao,
 18. 18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
 19. 19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
 20. 20. Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
 21. 21. Naye atakuja ridhika!