Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Al-Masad

111 – AL – MASAD

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

  1. 1. Imeangamia mikono ya Abu Lahab,nayeye pia ameangamia. 
  2. 2. Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
  3. 3. Atauingia Moto wenye mwako.
  4. 4. Na mkewe, mchukuziwakuni, 
  5. 5. Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.