Quran in Swahili
Al-Mursalât
77 – AL – MURSALAAT
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
- 2. Na zinazo vuma kwa kasi!
- 3. Na zikaeneza maeneo yote!
- 4. Na zinazo farikisha zikatawanya!
- 5. Na zinazo peleka mawaidha!
- 6. Kwa kuudhuru au kuonya,
- 7. Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
- 8. Wakati nyota zitakapo futwa,
- 9. Na mbingu zitakapo pasuliwa,
- 10. Na milima itakapo peperushwa,
- 11. Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
- 12. Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
- 13. Kwa siku ya kupambanua!
- 14. Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
- 15. Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
- 16. Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
- 17. Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
- 18. Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
- 19. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 20. Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
- 21. Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
- 22. Mpaka muda maalumu?
- 23. Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
- 24. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 25. Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
- 26. Walio hai na maiti?
- 27. Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
- 28. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 29. Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
- 30. Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
- 31. Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
- 32. Hakika Moto huo unatoa machechekamamajumba!
- 33.Kamakwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
- 34. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 35. Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
- 36. Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
- 37. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
- 38. Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
- 39. Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
- 40. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
- 41. Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
- 42. Na matunda wanayo yapenda,
- 43. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
- 44. Hakika ndiokamahivyo tunavyo walipa watendao mema.
- 45. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 46. Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
- 47. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 48. Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
- 49. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- 50. Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?