Quran in Swahili Al-Qadr 97 – AL – QADRKWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur’ani katika Laylatul Qadri, UsikuwaCheo Kitukufu. 2. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?3. Laylatul Qadrinibora kuliko miezi elfu. 4. Huteremka MalaikanaRoho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. 5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.