101 – AL – QAARIA’H
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Inayo gonga!
- 2. Nini Inayo gonga?
- 3. Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
- 4. Siku ambayo watu watakuwakamanondo walio tawanyika;
- 5. Na milima itakuwakamasufi zilizo chambuliwa!
- 6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
- 7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
- 8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
- 9. Huyo maskani yake yatakuwa MotowaHawiya!
- 10. Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
- 11. Ni Moto mkali!