
Quran in Swahili
Al-Qiyâmah
75 – AL – QIYAMAH
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. NinaapakwaSiku ya Kiyama!
- 2. Na ninaapakwanafsi inayo jilaumu!
- 3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
- 4. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
- 5. Lakini mtu anataka tu kuendeleanamaasi kwa siku zilioko mbele yake.
- 6. Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
- 7. Basi jicho litapo dawaa,
- 8. Na mwezi utapo patwa,
- 9. Na likakusanywa juanamwezi,
- 10. Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
- 11. La! Hapana pa kukimbilia!
- 12. Siku hiyo pa kutuanikwa Mola wako Mlezi tu.
- 13. Siku hiyo ataambiwa aliyo yatangulizanaaliyo yaakhirisha.
- 14.Balimtu ni hoja juu ya nafsi yake.
- 15. Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
- 16. Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
- 17. Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
- 18. Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
- 19. Kisha ni juu yetu kuubainisha.
- 20. Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
- 21. Na mnaacha maisha ya Akhera.
- 22. Zipo nyuso siku hiyo zitao ng’ara,
- 23. Zinamwangallia Mola wao Mlezi.
- 24. Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
- 25. Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
- 26. La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
- 27. Na pakasemwa: Nani wa kumganga?
- 28. Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
- 29. Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
- 30. Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
- 31. Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.
- 32. Bali alikanusha, na akageuka.
- 33. Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
- 34. Ole wako, ole wako!
- 35. Kisha Ole wako, ole wako!
- 36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
- 37. Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
- 38. Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
- 39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
- 40. Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?