94 – ASH-SHARH’
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Hatukukunjulia kifua chako?
- 2. Na tukakuondolea mzigo wako,
- 3. Ulio vunja mgongo wako?
- 4. Na tukakunyanyulia utajo wako?
- 5. Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
- 6. Hakika pamojanauzito upo wepesi.
- 7. Na ukipata faragha, fanya juhudi.
- 8. Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.