99 – AZ-ZILZALAH
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Itakapo tetemeshwa ardhikwamtetemeko wake!
- 2. Na itakapo toa ardhi mizigo yake!
- 3. Na mtu akasema: Ina nini?
- 4. Siku hiyo itahadithia khabari zake.
- 5. Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
- 6. Siku hiyo watu watatokakwamfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
- 7. Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
- 8. Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!