
Quran in Swahili
An-Naba’
78 – ANNABAA
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. WANAULIZANA nini?
- 2. Ile khabari kuu,
- 3. Ambayo kwayo wanakhitalifiana.
- 4. La!Karibu watakuja jua.
- 5. Tena la!Karibu watakuja jua.
- 6. Kwani hatukuifanya ardhikamatandiko?
- 7. Na milimakamavigingi?
- 8. Na tukakuumbeni kwa jozi?
- 9. Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
- 10. Na tukaufanya usiku ni nguo?
- 11. Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
- 12. Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
- 13. Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
- 14. Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,
- 15. Ili tutoe kwayo nafaka na mimea,
- 16. Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.
- 17. Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
- 18. Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,
- 19. Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango,
- 20. Na milima itaondolewa na itakuwakama
- 21. Hakika Jahannamu inangojea!
- 22. Kwa walio asi ndio makaazi yao,
- 23. Wakae humo karne baada ya karne,
- 24. Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
- 25. Ila maji yamoto sana na usaha,
- 26. Ndio jaza muwafaka.
- 27. Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
- 28. Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
- 29. Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
- 30. Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
- 31. Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu,
- 32. Mabustani na mizabibu,
- 33. Na wake walio lingana nao,
- 34. Na bilauri zilizo jaa,
- 35. Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo –
- 36. Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
- 37. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake!
- 38. Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
- 39. Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi.
- 40. Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!