114 – ANNAS
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Sema: NinajikingakwaMola Mlezi wa wanaadamu,
- 2. Mfalme wa wanaadamu,
- 3. Mungu wa wanaadamu,
- 4. Nashari ya wasiwasi waShetani, Khannas,
- 5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,
- 6. Kutokananamajini na wanaadamu.