Quran in Swahili
Ar-Rahmân
55 – ARRAH’MAN
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Arrah’man, MwingiwaRehema
- 2. Amefundisha Qur’ani.
- 3. Amemuumba mwanaadamu,
- 4. Akamfundisha kubaini.
- 5. Juanamwezi huenda kwa hisabu.
- 6. Na mimea yenye kutambaa,namiti, inanyenyekea.
- 7. Na mbingu ameziinua,naameweka mizani,
- 8.Ilimsidhulumu katika mizani.
- 9. Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
- 10. Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
- 11. Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
- 12. Na nafaka zenye makapi, na rehani.
- 13. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
- 14. Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
- 15. Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
- 16. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
- 17. Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
- 18. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 19. Anaziendesha bahari mbili zikutane;
- 20. Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
- 21. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 22. Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
- 23. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 24. Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwakama
- 25. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 26. Kila kilioko juu yake kitatoweka.
- 27. Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
- 28. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 29. Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
- 30. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 31. Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
- 32. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 33. Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
- 34. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 35. Mtapelekewa muwako wa moto nashaba; wala hamtashinda.
- 36. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 37. Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
- 38. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 39. Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
- 40. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 41. Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
- 42. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 43. Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
- 44. Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
- 45. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 46. Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
- 47. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 48. Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
- 49. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 50. Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
- 51. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 52. Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
- 53. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 54. Wawe wameegemea matandiko yenye bit’ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
- 55. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 56. Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
- 57. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 58. Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
- 59. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
- 60. Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
- 61. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 62. Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
- 63. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 64. Za kijani kibivu.
- 65. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 66. Na chemchem mbili zinazo furika.
- 67. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 68. Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
- 69. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 70. Humo wamo wanawake wema wazuri.
- 71. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 72. Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
- 73. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 74. Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
- 75. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 76. Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
- 77. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- 78. Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.