Quran in Swahili
Ash-Shams
91 – ASH-SHAMS
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Naapa kwa jua na mwangaza wake!
- 2. Na kwa mwezi unapo lifuatia!
- 3. Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
- 4. Na kwa usiku unapo lifunika!
- 5. Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
- 6. Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
- 7. Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
- 8. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
- 9. Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
- 10. Na hakika amekhasiri aliye iviza.
- 11. Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
- 12. Alipo simama mwovu wao mkubwa,
- 13. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
- 14. Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
- 15. Wala Yeye haogopi matokeo yake.