
Quran in Swahili
Ash-Shuʽarâ’
26 – ASH-SHUA’RAA
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. T’aa Siin Miim.(T’.S.M.)
- 2. HiziniAya za Kitabu kinacho bainisha.
- 3. Huenda labda ukajikera nafsi yakokwakuwa hawawi Waumini.
- 4. Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao.
- 5. Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutokakwaArrahman ila wao hujitenga nao.
- 6. Kwa yakini wamekanusha;kwahivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha.
- 7. Je!Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri?
- 8. Hakika katika haya zipo Ishara.Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
- 9. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 10. Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fikakwawatu madhaalimu,
- 11. Watuwa Hawaogopi?
- 12. Akasema: Hakikamiminachelea wasinikanushe.
- 13. Na kifua changu kina dhiki,naulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun.
- 14. Na wao wana kisasi juu yangu,kwahivyo naogopa wasije kuniuwa.
- 15. Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeninamiujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.
- 16. Basi mfikieni Firauninamwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 17. Waachilie WanawaIsraili wende nasi.
- 18. (Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni,naukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?
- 19. Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasionashukrani?
- 20. (Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea.
- 21. Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu,naakanijaalia niwe miongoni mwa Mitume.
- 22. Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia,nawewe umewatia utumwani Wana wa Israili?
- 23. Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mleziwawalimwengu wote?
- 24. Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyiniwenye yakini.
- 25. (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
- 26. (Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi,naMola Mlezi wa baba zenu wa kwanza.
- 27. (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenuni
- 28. (Musa) akasema: Ndiye Mola MleziwaMashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini.
- 29. (Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.
- 30. Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?
- 31. Akasema: Kilete basi,kamawewe ni katika wasemao kweli.
- 32. Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri.
- 33. Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao.
- 34. (Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu.
- 35. Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani?
- 36. Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo.
- 37. Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu.
- 38. Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu.
- 39. Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika?
- 40. Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda.
- 41. Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda?
- 42. Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele.
- 43. Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa.
- 44. Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda.
- 45. Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua.
- 46. Hapo wachawi walipinduka wakasujudu.
- 47. Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 48. Mola Mlezi wa Musa na Harun.
- 49. (Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote.
- 50. Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
- 51. Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini.
- 52. Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa.
- 53. Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo.
- 54. (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo.
- 55. Nao wanatuudhi.
- 56. Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari.
- 57. Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem,
- 58. Na makhazina, na vyeo vya hishima,
- 59. Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.
- 60. Basi wakawafuata lilipo chomoza jua.
- 61. Na yalipo onana majeshi mawili haya, watuwa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
- 62. (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!
- 63. Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.
- 64. Na tukawajongeza hapo wale wengine.
- 65. Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
- 66. Kisha tukawazamisha hao wengine.
- 67. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini.
- 68. Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 69. Na wasomee khabari za Ibrahim.
- 70. Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
- 71. Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.
- 72. Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
- 73. Au yanakufaeni, au yanakudhuruni?
- 74. Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.
- 75. Je! Mmewaona hawa mnao waabudu-
- 76. Nyinyi na baba zenu wa zamani?
- 77. Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 78. Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa,
- 79. Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.
- 80. Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.
- 81. Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.
- 82. Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo.
- 83.83, Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema.
- 84. Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye.
- 85. Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema.
- 86. Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu.
- 87. Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa.
- 88. Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.
- 89. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.
- 90. Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu.
- 91. Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu.
- 92. Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu
- 93. Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe?
- 94. Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
- 95. Na majeshi ya Ibilisi yote.
- 96. Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:
- 97. Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri,
- 98. Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 99. Na hawakutupoteza ila wale wakosefu.
- 100. Basi hatuna waombezi.
- 101. Wala rafiki wa dhati.
- 102. Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini.
- 103. Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
- 104. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 105. Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume.
- 106. Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?
- 107. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
- 108. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini mimi.
- 109. Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 110. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini mimi.
- 111. Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?
- 112. Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
- 113. Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
- 114. Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
- 115. Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri.
- 116. Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
- 117. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
- 118. Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.
- 119. Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni.
- 120. Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
- 121. Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini.
- 122. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 123. Kina A’d waliwakanusha Mitume.
- 124. Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
- 125. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
- 126. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini mimi.
- 127. Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 128. Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
- 129. Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!
- 130. Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
- 131. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini.
- 132. Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
- 133. Amekupeni wanyama wa kufuga na wana.
- 134. Na mabustani na chemchem.
- 135. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
- 136. Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha.
- 137. Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani.
- 138. Wala sisi hatutaadhibiwa.
- 139. Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
- 140. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 141. Kina Thamud waliwakanusha Mitume.
- 142. Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu?
- 143. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
- 144. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini.
- 145. Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 146. Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
- 147. Katika mabustani, na chemchem?
- 148. Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
- 149. Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
- 150. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini mimi.
- 151.151, Wala msit’ii amri za walio pindukia mipaka,
- 152. Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi.
- 153. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa.
- 154. Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
- 155. Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.
- 156. Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa.
- 157. Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta.
- 158. Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
- 159. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 160. Watu wa Lut’i waliwakanusha Mitume.
- 161. Alipo waambia ndugu yao, Lut’i: Je! Hamumchimngu?
- 162. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.
- 163. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit’iini mimi.
- 164. Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 165. Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?
- 166. Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!
- 167. Wakasema: Ewe Lut’i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!
- 168. Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu.
- 169. Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.
- 170. Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,
- 171. Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
- 172. Kisha tukawaangamiza wale wengine.
- 173. Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa.
- 174. Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
- 175. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
- 176. Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume.
- 177. Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?
- 178. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
- 179. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini mimi.
- 180. Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 181. Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.
- 182. Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;
- 183. Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi.
- 184. Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia.
- 185. Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa.
- 186. Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo.
- 187. Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
- 188. Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda.
- 189. Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.
- 190. Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
- 191. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 192. Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- 193. Ameuteremsha Roho muaminifu,
- 194. Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,
- 195. Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.
- 196. Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.
- 197. Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?
- 198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,
- 199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
- 200. Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu.
- 201. Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu.
- 202. Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari.
- 203. Na watasema: Je, tutapewa muhula?
- 204. Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
- 205. Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,
- 206. Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
- 207. Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
- 208. Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji –
- 209. Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
- 210. Wala Mashet’ani hawakuteremka nayo,
- 211. Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
- 212. Hakika hao wametengwa na kusikia.
- 213. Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa.
- 214. Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
- 215. Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini.
- 216. Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda.
- 217. Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- 218. Ambaye anakuona unapo simama,
- 219. Na mageuko yako kati ya wanao sujudu.
- 220. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
- 221. Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet’ani?
- 222. Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
- 223. Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo.
- 224. Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata.
- 225. Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?
- 226. Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?
- 227. Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.