102 – AT-TAKAATHUR
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
- 2. Mpaka mje makaburini!
- 3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
- 4.4, Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
- 5. Sivyo hivyo! Lau mngeli juakwa ujuzi wayakini,
- 6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
- 7. Tena, bila ya shaka, mtaionakwajicho la yakini.
- 8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.