Quran in Swahili
At-Târiq
86 – ATT’AARIQ
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
- 2. Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
- 3. Ni Nyota yenye mwanga mkali.
- 4. Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
- 5. Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
- 6. Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
- 7. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
- 8. Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
- 9. Siku zitakapo dhihirishwa siri.
- 10. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
- 11. Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
- 12. Na kwa ardhi inayo pasuka!
- 13. Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
- 14. Wala si mzaha.
- 15. Hakika wao wanapanga mpango.
- 16. Na Mimi napanga mpango.
- 17. Basi wape muhula makafiri – wape muhula pole pole.