95 – AT-TIN
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Naapa kwa tini na zaituni!
- 2. Na kwa Mlima wa Sinai!
- 3. Na kwa mji huu wenye amani!
- 4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
- 5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
- 6. Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
- 7. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
- 8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?