
Quran in Swahili
Az-Zukhruf
43 – AZZUKHRUF
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. H’a Mim
- 2. NaapakwaKitabu kinacho bainisha.
- 3. Hakika Sisi tumeifanya Qur’anikwaKiarabu ili mfahamu.
- 4. Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu,nitukufu na yenye hikima.
- 5. Je! Tuache kukukumbusheni kabisakwakuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa ukafiri?
- 6. Na Manabii wangapi tuliwatumakwawatu wa zamani!
- 7. Na hawajii Nabii yeyoteilawalikuwa wakimkejeli.
- 8. Na tuliwaangamiza walio kuwananguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita.
- 9. Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingunaardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi,
- 10. Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko,naakakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka.
- 11. Na ambaye ndiye aliye teremsha kutoka mbinguni majikwakiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyo kufa.Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa.
- 12. Na ambaye ndiye aliye umba katika kila kitu jikenadume, na akakufanyieni marikebu na wanyama mnao wapanda.
- 13. Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juuyao namseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeli weza kufanya haya wenyewe.
- 14. Na hakika sisi tutarudikwaMola wetu Mlezi.
- 15. Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanaadamunimtovu wa fadhila aliye dhaahiri.
- 16. Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo viumba,naakakuteulieni nyinyi watoto wanaume?
- 17. Na anapo bashiriwa mmoja waokwa yalealiyo mpigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira.
- 18. Ati aliye lelewa katika mapambo,nakatika mabishano hawezi kusema kwa bayana…?
- 19. Na wakawafanya Malaika, ambaoni waja wa Mwingi waRehema, ni wanawake!Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao?Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!
- 20. Nao husema: Angeli penda MwingiwaRehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ilakusema uwongo tu!
- 21. Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi,naikawa wao wanakishikilia hicho?
- 22.Baliwanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao.
- 23. Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.
- 24. Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa.
- 25. Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio kadhibisha!
- 26. Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu,
- 27. Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.
- 28. Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.
- 29.Balituliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliye bainisha.
- 30. Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.
- 31. Na walisema: Kwa nini Qur’ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?
- 32. Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhiyaojuu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.
- 33. Na lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli wajaalia wanao mkufuru Rahmani wana nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazo pandia,
- 34. Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake,
- 35. Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu.
- 36. Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet’ani kuwa ndiye rafiki yake.
- 37. Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.
- 38. Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe!
- 39. Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.
- 40. Je! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi?
- 41. Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao.
- 42. Au tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.
- 43. Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka.
- 44. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.
- 45. Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah’mani?
- 46.46, Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!
- 47. Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka.
- 48. Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.
- 49. Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.
- 50. Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.
- 51. Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni?
- 52. Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?
- 53. Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?
- 54. Basi aliwachezea watu wake, na wakamt’ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu.
- 55. Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote!
- 56. Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.
- 57. Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele.
- 58. Wakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu.Balihao ni watu wagomvi!
- 59. Hakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliye mneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili.
- 60. Na tungeli penda tungeli wafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana.
- 61. Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
- 62. Wala asikuzuilieni Shet’ani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhaahiri.
- 63. Na alipo kuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimekujieni na hikima, na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyo khitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnit’ii mimi.
- 64. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
- 65. Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao walio dhulumu kwa adhabu ya siku chungu.
- 66. Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?
- 67. Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachamngu.
- 68. Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika.
- 69. Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu.
- 70. Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo.
- 71. Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.
- 72. Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
- 73. Mnayo humo matunda mengi mtakayo yala.
- 74. Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.
- 75. Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.
- 76. Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu.
- 77. Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!
- 78. Kwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.
- 79. Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha.
- 80. Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong’ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.
- 81. Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu.
- 82. Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A’rshi, na hayo wanayo msifia.
- 83. Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo ahidiwa.
- 84. Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi.
- 85. Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa.
- 86. Wala hao mnao waomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki, na wao wanajua.
- 87. Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa?
- 88. Na usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini.
- 89. Basi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua.