Quran translations in many languages

Quran in Swahili

Quraysh

106 – QURAISH

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 

 

  1. 1. Kwa walivyo zoea Maqureshi,
  2. 2. Kuzoea kwao safari za siku za baridinasiku za joto. 
  3. 3. Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii,
  4. 4. Ambaye anawalisha wasipate njaa,naanawalinda na khofu.