Quran in Swahili
ʽAbasa
80 – A’BASA
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Alikunja kipaji na akageuka,
- 2. Kwa sababu alimjia kipofu!
- 3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
- 4. Au atawaidhika,namawaidha yamfae?
- 5. Ama ajionaye hana haja,
- 6. Wewe ndio unamshughulikia?
- 7. Na si juu yakokama
- 8. Ama anaye kujia kwa juhudi,
- 9. Naye anaogopa,
- 10. Ndio wewe unampuuza?
- 11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
- 12. Basi anaye penda akumbuke.
- 13. Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
- 14. Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
- 15. Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
- 16. Watukufu, wema.
- 17. Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
- 18. Kwa kitu gani amemuumba?
- 19. Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
- 20. Kisha akamsahilishia njia.
- 21. Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
- 22. Kisha apendapo atamfufua.
- 23. La! Hajamaliza aliyo muamuru.
- 24. Hebu mtu na atazame chakula chake.
- 25. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
- 26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
- 27. Kisha tukaotesha humo nafaka,
- 28. Na zabibu, na mimea ya majani,
- 29. Na mizaituni, na mitende,
- 30. Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
- 31. Na matunda, na malisho ya wanyama;
- 32. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
- 33. Basi utakapo kuja ukelele,
- 34. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
- 35. Na mamaye na babaye,
- 36. Na mkewe na wanawe –
- 37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
- 38. Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
- 39. Zitacheka, zitachangamka;
- 40. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
- 41. Giza totoro litazifunika,
- 42. Hao ndio makafiri watenda maovu.