Quran in Swahili
Al-ʽAdiyât
100 – AL – A’ADIYAAT
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
- 2. Na wakitoa motokwakupiga kwato zao chini,
- 3. Wakishambulia wakati wa asubuhi,
- 4. Huku wakitimua vumbi,
- 5. Na wakijitoma kati ya kundi,
- 6. Hakika mwanaadamunimtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
- 7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shakanishahidi wa hayo!
- 8. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupendamali!
- 9. Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
- 10. Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
- 11. Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwanakhabari zao wote!