Quran in Swahili
Al-Mutaffifin
83 – AL – MUT’AFFIFIIN
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- 1. Ole wao hao wapunjao!
- 2. Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
- 3. Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
- 4. Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
- 5. Katika Siku iliyo kuu,
- 6. Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
- 7. Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
- 8. Unajua nini Sijjin?
- 9. Kitabu kilicho andikwa.
- 10. Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
- 11. Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
- 12. Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
- 13. Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
- 14. Hasha!Baliyametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
- 15. Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
- 16. Kisha wataingia Motoni!
- 17. Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
- 18. Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I’liyyin.
- 19. Na nini kitakacho kujuvya nini I’liyyin?
- 20. Kitabu kilicho andikwa.
- 21. Wanakishuhudia walio karibishwa.
- 22. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
- 23. Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
- 24. Utatambua katika nyuso zao mng’aro wa neema,
- 25. Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
- 26. Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
- 27. Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
- 28. Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
- 29. Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
- 30. Na wanapo pita karibuyao
- 31. Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
- 32. Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
- 33. Na wao hawakutumwa wawe walinzi juuyao.
- 34. Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
- 35. Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
- 36. Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?